TSB yakutana na Timu ya Tathmini ya Msajili wa Hazina na ESRF

Imewekwa: 10 Feb, 2026
TSB yakutana  na Timu ya Tathmini ya Msajili wa Hazina na ESRF

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Bw. Saddy Kambona, ameiongoza Menejimenti ya Bodi katika kikao kilichohusisha Timu ya Tathmini kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).

Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Bodi ya Mkonge Tanzania (Mkonge House), jijini Tanga na kililenga kufanya tathmini ya utendaji kazi wa Bodi ya Mkonge Tanzania.

Aidha, kikao hicho ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuimarisha mifumo ya usimamizi, uwajibikaji pamoja na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi za umma.

Taasisi Shirikishi
Hakimiliki ©2026 Bodi ya Mkonge Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.