MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KATIKA TASNIA YA MKONGE

Imewekwa: 27 Jan, 2025
MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KATIKA TASNIA YA MKONGE

Bodi Ya Mkonge Tanzania inaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia.

Kupitia zao la Mkonge, wadau wanaweza kuzalisha nishati safi ya kupikia kwa kutumia mabaki ya Mkonge yanayopatikana baada ya kuchakata majani.

Mitambo ya gesi inayotumia mabaki ya Mkonge katika kuzalisha gesi ni imara, nafuu na inadumu kwa zaidi ya miaka 50.

Tunza mazingira, tumia nishati safi ya kupikia itokanayo na mabaki ya Mkonge.

Taasisi Shirikishi